Ikiwa ni siku moja baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu na Nusu jela Rais Wa Bayern Munich Uli Hoeness amejiuzulu nyadhifa zake zote ikwemo urais wa timu hiyo na uwenyekiti wake
Kujiuzulu huko kunatokana na kukutwa na kosa la kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha 27m euros,pia Bwana Hoeness amesema hatokata rufaa na yupo tayari kutumikia Adhabu hiyo kutokana na kukiri ya kwamba kosa la kukwepa kulipa kodi ni kosa kubwa na anajutia katika maisha yake yote
Hata hivyo bwana Hoeness amechukua fursa hiyo kuwashukuru mashabiki wa Bayern Munich na watu wote waliojitokeza kumsupport katika kipindi chote cha uchunguzi
Bwana Hoeness aliichezea timu hiyo katika kipindi cha mwaka 1970 mpaka 1979 na kuipatia ubingwa wa kombe la ulaya katika club hiyo na kombe la dunia akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya ujerumani magharibi kabla ya kustaafu kabla ya wakati akiwa na umri wa miaka 27 kwa majeruhi