
Katika hali ya kushangaza Mshiriki Mrembo kutoka Zimbabwe Pokello ameyaaga mashindano yaho bila ya kutegemea, Pokello ambaye amekuwa akitajwa kama mshiriki mwenye ushindani mkubwa ndani ya nyumba Ameyaaga mashindano baada ya kura zake zakumbakisha ndani ya nymba kuwa chache, Mara zote Pokello alipokuwa kikaangoni alikua anaokolewa na kura nyingi sana toka kwa watazamaji lakini ili kuona kuwa mchezo huo hautabiriki leo hii Ametoka ,
Pokello akiagwa kutoka ndani ya nyumba na Rafiki yake kipenzi Elikem kutoka Ghana.
Hata hivyo imekuwa nafuu kwa mshiriki wetu kutoka Tanzania Feza ambaye alikuwa na biff la kiana na Pokello, kwa mujibu wa pokello baada ya kuulizwa swali juu ya machafuko yake na Feza alisema ya kuwa Feza ni msichana ambaye alionesha kutompenda tangu siku ya kwanza walipoingia katika nyumba na ndo maana hata aliweza kumuweka kikaangoni siku Feza alipokua mkuu wa nyumba, Pokello anasema kikubwa alichokiona ni kwamba Feza alikua anamuogopa kwa kuwa alikuwa mshindani wake mkubwa, Hata hivyo pokello alimuambia MC IK kuwa anaamini Feza atakuwa na raha sasa kwasababu ametoka.
Bassey Kutoka Siera Lione Akiagwa toka ndani ya nyumba
Mshiriki mwingine aliyoyaaga mashindano hayo leo ni Bassey mshiriki kutoka Sierra Lione ambaye ndio alikuwa wa kwanza kutajwa kutoka ndani ya nyumba hiyo.
Wengine waliokuwa kikaangoni na wameokoka mara hii ni pamoja na Mshiriki Annabel kutoka Kenya, Dillish kutoka Namibia, Angelo kutoka Afrika Kusini
Ahsante Afrika mashariki kwa kumuokoa Annabel Tufanye hivyo kila washiriki wetu kutoka Afrika mashariki wanapokuwa kikaangoni.
Hivi ndivyo Afrika ilivyopiga Kura
