Kampuni ya Apple inatumaini huduma ya music streaming ya Dr. Dre itaongeza mauzo. Beats Music imepangwa kuzindua tena ikiwa ni sehemu ya iTunes kwa mwaka ujao, Allhiphop inaripoti kwamba mipakuo ya iTunes (downloads) imeshuka na Apple inatumaini kwa kuungana kwa huduma ya streaming itaongeza mapato. Tovuti hiyo imeeleza kupitia article iliyoandika kwa Wall Street Journal ambalo lilisema mauzo muziki kwenye iTunes yameshuka kwa asilimia 3 hadi 14 duniani kote toka mwaka huu umeanza. Dr. Dre na Jimmy Ioine walizindua Beats Music mwezi Januari na ilikuwa na maana ya kushindana na huduma ya music streaming kama Spotify na Pandora, Kutumia huduma ya Beats Music inagharimu dola
9.99 kwa mwezi. Mwezi Mei, Apple ilinunua Beats Electronic na Beats Music, Dili hiyo iliripotiwa kuwa na thamani ya dola bilioni 3, bei ilikatwa kutoka dola biliono 3.2 kwa sababu ya watumiaji wachache wa Beast Music. Beats Music waligonga vichwa vya habri mwaka huu tena baada ya NFL National Football League kutaka wachezaji wavae bidhaa nyingine na sio za Beats Music, wachezaji walitakiwa wasivae headphones hizo kwenye michezo na dakika 90 kabla ya michezo kuanza. Mchezaji wa San Francisco 49ers Colin Kaepernick alikuwa na deal na Beats na alipigwa faini ya dola 10,000 kwa kuvaa headphones zake kwenye mkutano na wandishi wa habari baada ya mchezo. Cam Newton, Richard Sherman na Tom Brady pia wamekuwa wakionekana wakivaa Beats heaphones kwenye uwanja toka katazo hilo lilipotolewa.