“Inatakiwa Uwe Mwanajeshi Kwenye Mapenzi” Jada Pinket Atoa Siri Iliyosababisha Kuwa Na Ndoa Kwa Miaka 18 Yenye Mafanikio Na Will Smith
Jada Pinkett n Will Smith wameoana miaka 18 iliyopita ilikuwa Desemba 31 1997, Jada alipoulizwa siri ya kudumu na kuwa na mafanikio katika ndoa yao ingawa kulikuwa na uvumi wa wawili hao kuachana aliiambia FOX kwamba
“Mpenzi wako anatakiwa awe rafiki yako kipenzi, na Will na rafiki yangu mkubwa, Inatakiwa uwe na akili ya kishujaa, inatakiwa uwe mwanajeshi kwa ajili ya mapenzi, inatakiwa uweze kuvuka muda ambao mambo hayaendi vizuri, ikifika muda mambo sio haimaanishi kwamba ni muda wa kuacha, huo ndo muda wa kupigana, Tunakwenda kusherekea miaka 20 ndani ya miaka miwili ijayo, kwa hiyo tunaanza kujipanga kwa ajili ya kitu kikubwa kama hiki cha miaka 20 ya ndoa yetu” Alisema Jada.
Katika maisha mambo ni mengi katika ndoa lakini inabidi tushindane na vitu vinavyokuwa vinatokea kiukweli huwa kuna magumu sana katika ndoa, ndo maana watu wengine wanakaa miezi tu wanaachana, wengine mwaka tu wanaachana, miaka 18 sio mchezo katika ndoa.
If the wall could speak lakini ndo ivyo kuwa rafiki wa mume wako au mke wako muangalie kitu gani mtafanya ili muweze kuendelea kwa sababu kuachana sio suluhisho la matatizo utaenda sehmu nyingine utakutana na mengine zaidi ya kule ulipotoka.
Ni kuwa wanajeshi katika ndo zetu.