
Jana Juma pili 14/07 Ilikua Evection show nyingine kutoka ndani ya Jumba la Big Brother the Chase ambapo washiriki kutoka Malawi Natasha Na Selly wa Ghana waliyaaga mashindani hayo.
Natasha kama alivyokuwa anafahamika zaidi kama mama Africa kutokana na kuwa katika mandhari ya kiafrika muda mwingi pia umbile lake na jinsi alivokua anaishi ndani ya jumba hilo aliweza kujikusanyia mashabiki wengi kitu kilichomfanya awe anaviruka vihunzi kila alipokuwa kikaangona lakini kwa bahati mbaya mara hii akanasa mtego na hatimae kuyaaga mashindano.
Selly kutoka ghana hakupigiwa kura za kutoka na washiriki wenzake lakini alitolewa kafara na mkuu wa nyumba ya Ruby ambaye ni Shemeji yetu kwa Tanzania O’neil kutoka botswana. Selly pia tunaweza kusema alikua shemeji yetu wa mpito baada ya kuruhusu Apple lake kufanywa one night stand na mshiriki Nando wa Tanzania siku za mwanzoni mwanzoni, Japo penzi hilo halikuendele kutokana Ukweli ya kwamba Nando hakuwa na mapenzi na Binti huyo kutoka Afrika Magharibi Selly. Macho ya Nando yanaonekana zaidi kumvizia Dilish Kutoka namibia .
kikubwa na kizuri kwa Watanzania ni kwamba Bado Tanzania imeendelea kupeta kutokana na washiriki wake kuwa safe mpaka wakati huu ambao washiriki wa nyumba ya Ruby na Diamond watachanganywa katika nyumba moja… haijajulikana kama leo usiku jumatatu 15/07 Zile kura zitapigwa toka kwa washiriki au kuna kusubiria mchanganyiko huo. update zaidi kesho jumanne.
Hata hivyo katika kunogesha mchezo zaidi Big Brother Amewaleta washiriki feki kutoka
alivyoiita mwenyewe katika kuwachanganya washiriki halali ili kuufanya mchezo uvutie zaidi…. Watazamaji hawatawapigia kura washiriki feki kwamaana wao wapo kuwa stress tu washiriki halali.
Hawa ndio washiriki wengine waliyokuwepo kikaangoni wiki iliyopita na jinsi Afrika ilivyopiga Kura
Namibia: Melvin
Nigeria: Melvin
South Africa: Pokello
Sierra Leone: Melvin
Tanzania: Annabel
Uganda: Annabel
Zambia: Cleo
Zimbabwe: Pokello
Rest of Africa: Melvin
Total: Melvin = 5; Annabel = 3; Cleo = 2, Pokello = 2, Natasha = 2, Selly = 1. (Total: 15 Votes)
Please Note: The tie breaker rules were applied Pokello, Natasha and Cleo as they each had two popularity votes, the Housemate with the lowest average percentage across all countries was Natasha.
Katika hatia nyengine humo humo ndani ya jumba la kaka Mkubwa Mshiriki Wa Tanzania Feza Ameonyesha u serious katika mahusiano yake na Mshiriki wa Botswana O’neil baada ya kumuweka wazi mpezi wake huyo kuwa anachokihitaji kutoka kwake ni Mapenzi ya ukweli, Future,Maisha na watoto, maongezi yaliofanyika katika section ya chumba maalum.
tusubiri kuona ni mchezo tu au anamaanisha.
