Wakati alipokuwa akitweet matukio ya furaha wakati wa kombe la dunia, haikuwa bila sababu, Shabiki huyo wa mpira ambaye ni mwanamuziki maarufu duninai mwenye vimbwanga!! Riri anataka kuanzisha chuo cha mpira wa miguu huko kwao Barbados na pia anaongea kuhusu kununua klabu ya mpira. Kwa sasa kuna taarifa kwamba Riri anaitolea macho Liverpool FC.
El Mundo Deportivo imetoa taarifa kwamba Rihanna ameshauriwa na rafiki yake mzuri star wa Chelsea Didier Drogba.
Chanzo kimoja cha karibu kimesema
“Mara ya kwanza alidhani Rihanna anatamani kujihusisha na mpira kibiashara tu kawaida tukadhani bado ana mzuka wa kombe la dunia, lakini sasa inakuwa wazi kweli anamaanisham anaongea kuhusu kuanzisha chuo cha mpira katika taifa lake la Barbados…
Pia ndoto yake kubwa ni kujihusisha na klabu kubwa nchini Uingereza, sisi tunasikilizia tu kwa sababu Rihanna ameshatengeneza mkwanja mrefu sana hadi sasa she can do whetever, juzi tu amepiga picha kwa ajili ya W Magazine na pale amevuta mkwanja pia, tour Monster nayo imevuna mkwanja kwanini asiinvest sasa kwenye kitu cha maana, Jay Z yeye aliwekeza kwenye mpira wa kikapu kwa sababu ndo anapenda alinunua Brookly Net.
Mpira wa miguu ni biashara nzuri kwa sababu ndio mchezo unaongoza kwa kuwa namashabiki wengi duniani kote kwa hiyo akiingia huko sidhani kama Rihanna atafilisika kama inavyowatokea mastaa wengine duniani.