Watu wengi hawakupata nafasi ya kuona jinsi ilivyokuwa katika harusi ya Kanye West na Kim Kardashian, ni kama Jay Z na Beyonce ambao kwa mara ya kwanza juzi wakiwa Miami katika tamasha la On run tour ndo walionyesha picha za harusi yao, Kwa Kanye West picha zimeonekana lakini kilichotokea pale iliikuwaje ndo watu wengi hawakupata nafasi ya kuona lakini ipo siku itatoka video trust me.
Mkali kutoka kampuni ya GOOD MUSIC BIG Sean alikuwepo na amesema harusi ilikuwa noma, akiongea kuhusu harusi ya Boss wake Boss Good Music Big sean alifunguka wakati akipiga stories na The Breakfast Club sehemu inafahamika kama KUBE 93 alisema ilikuwa ni classic ilikuwa kama harusi ya familia ya kifalme, helikopta ilikuwa ikizunguka katika eneo hilo.
Big Sean pia akaongelea kukuta na Chriss Brown baada ya kutoka jela amesema mshikaji amenenepa alimuuliza nini ulikuwa unapata jela na akasema wana ngoma wanafanya itatoka siku zijazo.
Big Sean na Chriss Brown walishafanya ngoma inaitwa My last ilikuwa tight sana, wana chemistry nzuri wakifanya ngoma napenda wakifanya ngoma.