Siku moja wakati akipiga stories na Mtandao wa Times alitania kutokuwa na mtoto inaweza ikawa sababu ambayo ilimsababisha aishi muda mrefu kutokana na kutopoteza nguvu nyingi.
Mzee huyo aliyekuwa na umri wa miaka 111 alizaliwa Februari 4 mwaka 1903 nchini Poland, alikulia Czestochowa huko kaskazini mwa Poland, yeye na mke wake wa pili anaeitwa Wela , walihamia Waterbury Conn mwaka 1951,Baada ya kifo cha mke wake Wela Imich akahamia New York mwaka 1986.
Sakari Momoi ni Mjapani mwenye umri wa miaka 111 ambaye alizaliwa siku moja mbele baada ya Imich kwa sasa inaaminika ndio Mwanaume mwenye umri mkubwa dunia Bwana Sakari Momoi lakini kwanza wataalamu wanatakiwa kuthibitisha umri wake.
Kulingana na utafiti wa kikundi cha Gerontology wamesema kuna wanawake 66 wenye umri mkubwa kuliko Momoi akiwemo mwanamke Mjapani Misao Okawa mwenye umri wa miaka 116.