Msanii rais wa ghetto Mheshimiwa Bob Wine hatimaye ameamua kumuacha aende meneja wake wa siku nyingi wa mambo ya biashara Bwana Labeja Laurence katika Fire base entertainment. Kwa hiyo kwa sasa mambo yote ya kibiashara kuhusu Bob wine, bookings na maulizo yeyote yatakuwa yakielekezwa moja kwa moja katika makao makuu ya ofisi za Fire Base Entertainment yaliyopo Semakokilo Plaza kiwanja namba 240 barabara ya Kira Kamwokya huko Kampala. Bobi Wine ambae lisumbua na ngoma ya time bomb alinukuliwa akisema mwenyewe kupitia mitandao kwamba kufanya hivyo hakujachochea ubaya wowote au damu hazijaendana, Mr Labeja anaendelea kuwa mwanafamilia na rafiki na kaka, tunashukuru kwa support
ambazo mnaendelea kutoa. Hii inaonekana kama ni njia nzuri ya kumfukuza mtu, kila boss sehemu alipo atatakiwa amuige ghetto President Mheshimiwa Bob Wine. Unamfukuza mtu alafu unaendelea kusema bado ni mwanafamili, kaka na rafiki…si mbaya lakini the naked truth seen!!