Kwa mujibu wa Fox 5 News, Nyota wa muziki wa Pop Janet Jackson anakua muislam na ataacha muziki Rasmi
Taarifa za kituo hicho cha Televisheni zimesema kuwa baada ya mwanamama huyo kufunga ndoa na bilionea wa kiarabu, Wissan Al Mana, ameamua kuacha jumla kazi ya muziki
Janet Atahama Marekani na kuhamia Mashariki Ya Kati kwa mumewe na anasilimu na kuwa muislam, Ripoti ya kituo cha televisheni imesema hivyo.
Janet na Wissam wakifunga ndoa kwa siri mwaka jana na sasa wanajiandaa kuendelea na maisha yao ya faragha mbaki na macho ya watu.
Hili si tukio la kwanza kwa wanafamilia hawa wenye nguvu sana duniani kuslim, Hata marehemu Michael Jackson inasemekana Alislim Japo hakuweka wazi mpaka mauti yake lakini pia tunaona moja kati ya kaka mmoja wa Michael na Janet ni muumini mzuri wa Dini ya Kiislam