Aliyekuwa mbunge wa Chambani visiwani Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha CUF Mh. Salim Hemed Khamis (Pichani) amefariki dunia.
Taarifa zilizopatikana ni kuwa amefariki katika hospitali alikopelekwa baada ya kuanguka.Mbunge huyo wa Jimbo la Chambani aliugua ghafla wakati akihudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mh. Edward Lowassa na Makamu Mwenyekiti Mussa Hassan Zungu na baadhi ya wajumbe walimtoa nje ya ukumbi na kumpepea kwa kutumia magazeti na majarida.
Hata hivyo, hali yake ilizidi kuwa mbaya huku akizungumza kwa tabu kuwa alikunywa dawa za shinikizo la damu (BP) kabla hajala chochote na hivyo kuzidiwa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.