‘
Kama unakumbuka ngoma ya kwanza aliyofanya P.Diddy na sauti yake kusikika ilikuwa ni “Cant No Body Hold Me Down” akiwa na Mase na ngoma hiyo aliisample kutoka ngoma ya “Check your self” ya Ice Cube.
Baada ya kuwa P.Diddy ameshatengeneza hitz kibao akaona naye atishe kwa kuweka sauti kwenye ngoma hiyo ilikuwa mwaka 1996.
“Nilijua niliipenda ngoma hiyo, nilijua tayari nimeshatengeneza ngoma kibao zilizofanya vizuri, lakini sikuwa na ngoma yeyote iliyokuwa na sauti yangu, kwa hiyo katika mipango mikubwa ilikuwa ni jaribio langu na ikawa ndo formula ya mkongwe kama mimi” alisema P.Diddy kupitia Complex TV Magnum Opus series..
Ilikuwa ni kati ya ngoma zake anazozipenda, ahisi anaweza kufanya kitu fulani tofauti, ilikuwa sample kwa sababu ya tempo yake na speed, ilikuwa ikipigwa sana club mara kibao.
Na kilikuwa kitu ambacho kila mtu alikijua, kulikuwa na nafasi ya kufanya kitu kupitia wimbo ule na hii ilikuwa kipindi ambacho kila mtu alikuwa akifanya sampling na kutafuta sample kali.