Chama cha Mapinduzi, CCM kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa,
Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa ameibuka mshindi baada ya kuwabwaga wapinzani wake kutoka chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Bi Grace Tendega.
Godfrey Mgimwa amepata kura 22,962 akifuatiwa kwa mbali na mgombea Grace Mvanda wa CHADEMA aliyepata kura 5,853 ,
Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kalenga Dr.William Mgimwa, ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha wa Tanzania kufariki dunia.