Msemaji wa jimbo la Anambra nchini Nigeria Mike Uda ameiambia BBC kuwa wanaomboleza kifo cha wanayemwita mtoto wa taifa la Nigeria na Afrika kwa ujumla.Chinua Achebe alizaliwa mwaka 1930, miaka 30 kabla ya Nigeria kupata uhuru.
Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia yake, imemwelezea Chinua Achebe kuwa mmoja wa waandishi wakubwa wa vitabu vya fasihi katika kipindi chake, ambaye busara yake ilikuwa kichocheo cha kumwiga kwa wale wote waliomfahamu.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi daima katika mioyo ya akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo.
Alipata umaarufu mkubwa kutokana na utunzi wa kitabu chake cha kwanza cha fasihi kitwaacho ‘Things Fall Apart’, ambacho alikitunga mwaka 1958 kikizungumzia athari za ukoloni barani Afrika.
Kitabu hiki kiliuza zaidi ya nakala milioni 10. Things Fall Apart kimetafsiriwa katika zaidi ya lugha 50 na kuelekeza mtazamo wake katika jamii ya Wa-Igbo na mgongano wa kimaadili kati ya nchi za mgaharibi na kijadi.
Alipata ngazi ya uprofesa kutoka chuo kikuu cha Boston nchini Marekani mwaka 1970 ambapo katika siku za hivi karibuni alikuwa akikosoa baadhi ya mienendo mibaya ya serikali ya Nigeria.
Amekuwa akiishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 kufuatia kujeruhiwa katika ajali ya gari.Ameandika kazi za kitaaluma zaidi ya 20, baadhi zikikosoa vikali wanasiasa na uongozi mbaya nchini Nigeria.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi daima katika mioyo na akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo.
Chinua Achebe Muandishi Nguli Wa Vitabu Duniani Afariki huku dunia bado ikimuhitaji
Previous Story
KITAA
Related Posts
-
-
George W Bush Ni Miongoni Mwa Walioshiriki Kampeni Ya Kujimwagia Maji Ya Barafu (Ice Bucket Challenge), Barak Obama Kala Kona
-
Mwanafunzi wa Makongo Akabidhiwa Gari Lake Rasmi
-
Waziri Mkuu Mizengo Pinda Aagiza Kufanywa Kwa Ukaguzi Wa Kina Kwa Magari Yote Yanayoingizwa Nchini.
-
Nicki Minaj Ashinda Tuzo Ya People’s Choice Award
-
MAJAMBAZI YAVAMIA GARI NA KUPORA MAMILIONI JIJINI DAR LEO SAA TANO ASUBUHI
-
Wananchi Wa Kenya wasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu kesi ya ushindi wa Rais