Chriss Brown na mwanasheria wake ambae anashughulikia kesi yake ya Octoba ya shambulio nje ya hoteli huko Washington D.C walikuwa wakiomba kesi hiyo itupiliwe mbali lakini ombi lao halijaafikiwa.
Chriss Brown anaweza kwenda jela kwa sababu watetezi wake na waendesha mashataka kutokukubaliana kutokana na kile Chriss Brown atakachokisema kilitokea 2013 katika tukio hilo.
Muimbaji huyo imeripotiwa aliwasili inakadiriwa kuwa saa 10:30 alfajiri Octoba 27 na watu wawili wakataka kupiga nae picha mbele ya hoteli hiyo huko Washington D.C.
Ttaarifa za kisheria zinasema, Wakati watu hao wakijiandaa kupiga picha inasemekana Chriss Brown aliwashambulia kwa maneno machafu (gay slur) kabla ya kurusha ngumi kwa mmoja wao. Wakati tukio hilo likitokea Chriss Brown alikuwa bado ana kesi ya shambulio la 2009 la kumpiga mpenzi wake Rihanna na tukio la pale hotelini Washington D.C linaweza kuangaliwa kama kuvunja masharti ya kosa la kwanza hakutakiwa kufanya kosa lingiine wakati bado la kumpiga Rihanna lilikuwa halijaisha.
Kwa hiyo anaweza akaenda jela kwa muda wa miaka minne.
Muendesha mashtaka kwenye kesi hiyo jana Juni 25 amesema wamempa Chriss Brown na timu yake muda wa kujitetea kutokana na shambulio hilo na kuokoa muda taarifa kutoka AP zimeeleza.
Lakini imeshindikana kwa sababu pande zote mbili zimeshindwa kuafikiana kwa kile kilichotokea hotelini Washington D.C. “Walitaka asome kutoka kwenye script na hiyo haikuwa kweli” Mwanasheria wa Chriss Brown Mark Geragos alisema baada ya kusikilizwa kesi hiyo.