Chriss Brown amesema Kendrick Lamar ni kwere, noma sana, Chriss Brown alifanya na ngoma na Kendrick Lamr kwenye ngoma inaitwa “Autumn Leaves” na mkali huyo wa ngoma ya “loyal” anasema anaheshima kubwa kwa mkali wa albamu ya good kid, m.A.A.d. city Kendrick Lamar.
“Kendrick ni noma, nadhani ni mshikaji fresh pembeni ya kuwa msanii, ni mpole na anaheshima, na pia ni anaandika mashairi makali sana, kwa hiyo nadhani tuliporekodi, alichokisema kinahusika ni jinsi alivyoifanya ngoma ilikuwa ni nom asana, nadhani alikuwa na vesi kali ambayo nimewahi kusikia kwa kile alichokisema na ujumbe aliokuwa akiongelea” alisema Chriss Breezy wakati akipiga stories na XXL na Miranda J.
Chriss Brown anasema Lamar anajitofautisha na marepa wengine kutokana na mada anazoziweka katika mashairi yake.
“Marepa wengine, wanaongela vitu wanavyomiliki, au walivyovipata, au jinsi wanavyong’aa, lakini nadhani unaweza ukapaka rangi picha kimashairi, ina faida zaidin na mwishowa siku ina maana sana zaidi, na inaenda muda mrefu” aliongeza Chriss Brown.
Pia Taylor Swift alishasema akiwa na stress anamsikiliza Kendrick Lamar fresstyle.