Dj mkali anayeafanya vizuri kwa sasa nchini Tanzania na Africa Mashariki Dj Tass mkali wa video mixing (Dvj), pia ni host wa show kali Afrika Mashariki “Wakilisha” inayoruka Dstv Maisha Magic channel 161 kila siku za wiki Jumatatu mpaka Ijumaa, saa 10 hadi 11:00 jioni na Maisha Magic Swahili channel 158 saa 11 – hadi 12:00 jioni Jumatatu hadi Ijumaa. Ijumaa tarehe
14 Novemba 2014 atakuwa kwenye jumba
la Big Brother Africa msimu wa 9 almaarufu kama Hotshots, akitoka huko moja kwa moja akiwa official dj of BBA season 9 The Hotshots representing East Africa atatua ndani ya Savanna Lounge Benjamin Mkapa ghorofa ya 3 ili kuwarusha fans wake kwa mara ya kwanza akiwa na vibes za Big Brother Africa Season 9 Hotshots 2014.
Dj Tass pia ni dj wa fun and craziest afternoon show Dala Dala Beats @ Magic FM kipindi cha kila siku Jumatatu hadi Ijumaa saa 7 – 10:00 jioni na Kwetu Flava kipindi anachokifanya kila siku za Jumatatu mpaka Alhamisi saa 2:45 hadi saa 5:00 Usiku.
(Dj Tass na Diamond Platinumz wakiwa studio za Magic FM Dar es salaam 92.9)
Watanzani pia mnatakiwa kuendelea kumpigia kura mshiriki kutoka Tanzania Idris ili aibuke mshindi wa Big Brother Africa msimu huu wa 9 mwaka 2014.Kumpigia kura Idris mshiriki kutoka Tanzania andika neno “Vote Idris” kisha tuma kwenda namba 15426 . Unaweza kupiga kura mara nyingi uwezo ili kumwezesha kuwa mshindi, na Ijumaa hii Dj Mtanzania mwenzake anakwenda kumrusha yeye na washiriki wenginee kutoka nchi nyingine za Afrika ndani ya mjengo wa Big Brother Africa…Go! Tass, Go! Tass, Go! Tass #TURNUP