
DjQ akiwa na mwanae Cassim katika Ofisi za Magic Fm Leo
Mtangazani Wa Magic Fm Mohammed Chande au almarufu Dj Q amekutana na mtoto wake wa kiume Baada ya miaka 22. Mtoto huyo anayekwenda kwa jina la Cassim alizaliwa miaka ishirini na mbili iliyopita Huko Lindi sehemu ambapo Dj Q Ndipo alipozaliwa na kusomea.
Kwa Mujibu wa Dj Q mwenyewe Alikutana na mama wa mtoto huyo akiwa na umri wa miaka 17 wakati huo mama wa mtoto huyu naye alikua nwanafunzi, baada ya historia kujiandika Dj Q aliendelea na maisha yake na kuhamia jijini Dar Es Salaam katika harakati za kutafuta maisha ndipo kutoelewana kwa mzazi mwenzie kulipojitokeza na Mama kuamua kumlea mwanaye bila kumshirikisha Dj Q kwa muda wote huo wa miaka 22
DjQ akiwa na uso wa furaha kabisa baada ya kukutana na mwanaye Cassim
Hata hivyo Dj Q aliiambia salmamsangi.com ya kuwa yeye hakumkataa mtoto isipokua mama ndio alileta ubinafsi baada ya mapenzi kuisha
Na sasa DJ Q anafurahia kukutana na Mwanaye huyo huku akifurahia kuchukua majukumu yote yaliobakia katika kumsomesha katika masomo yake ya chuo anayoendelea nayo huko Dodoma
Pia Q alimalizia kwa kusema sasa ni wakati wa kumtambulisha mtoto wake kwa familia yake ikiwa ni pamoja na wadogo zake wengine watatu
