ALBERT MANGWEA WA KWANZA KULIA AKIWA NA MARAFIKI ZAKE NCHINI AFRIKA KUSINI SIKU CHACHE KABLA MAUTI KUMFIKA
TAARIFA YA KUFARIKI MSANII WA KIZAZI KIPYA ALBERT MANGWEA ITAKUA SIO NGENI MASIKIONI MWAKO, KWANI TAARIFA HIZI ZILISAMBAA KWA HARAKA SANA JANA JIONI BAADA TU YA TUKIO HILO KUJITOKEZA… TAARIFA KUTOKA KWA WATU WA KARIBU NA MSANII HUYO ALBERT MANGWEA NI KWAMBA ALIKUA NCHINI AFRIKA YA KUSINI AMBAPO ALIKWENDA KWAA AJILI YA SHOW KATIKA MJI WA PRETORIA NA ALIKUA HUKO TAKRIBANI KWA MUDA WA MIEZI MIWILI
Hii ndio hospitali alimofikishwa Msanii Albert Mangwea
MANGWEA AKIWA NA RAFIKIA YAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA M TO THE P AMBAYE NAE PIA INASEMAKANA NAYE YUPO MAHUTUTI AKIPUMULIA MASHINE
AKIWA NCHINI AFRIKA KUSINI ALIKAA KWA MARAFIKI ZAKE MMOJA AKIJULIKANA KAMA RAMA RASTA NA MWINGINE AMBAYE NAYE NI MWANAMUZIKI HUKO M TO THE P KATIKA MIJI YA PRETORIA NA JOHANNESBURG, SIKU YA JANA NDIO SIKU MANGWEA ALITAKIWA KURUDI NYUMBANI TANZANIA BAADA YA KUAHIRISHA SAFARI KWA AJILI YA COLABO ALIOTAKIWA KUIFANYA NA JAMAA MMOJA ANAYEISHI MJI UNAITWA KIMBERLY
HATA HIVYO INASEMEKANA USIKU WA KUAMKIA JANA SIKU YAKE YA SAFARI, KAMA AMBAVYO ILIKUA INAFAHAMIKA KUWA MSANII MAGWEA ALIKUA MTUMIAJI WA MIHADARATI TANGU KIPINDI CHA NYUMA SASA ALIJIKUTA AKICHANGANYA MADAWA TOFAUTI ALIYOKUA ANATUMIA BILA KUJIJUA NA HIYO IKAWA SABABU YA KUJI OVER DOZE
NA KUSABABISHA KUZIDIWA HATIMAE KUKIMBIZWA KATIKA HOSPITAL YA ST.HELLEN SAMBAMBA NA HUYO RAFIKI YAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA M TO THE P AMBAE WALITUMIA WOTE…. TAARIFA ZA AWALI ZILISEMA YA KUWA M TO THE P ALIKUWA MAHUTUTI LAKINI MPAKA MWANDISHI WA MTANDAO HUU ANAWEKA KALAMU CHINI HABARI ZILIZOPO NI KWAMBA NAYE YU MAHUTUTI AKIPUMULIA MASHINE AMBAYO ATAITUMIA KWA MASAA SABA TU NA BAADA YA HAPO KAMA HATA PUMUA MWENYEWE WATAMTOA MASHINE HIYO NA STORI ITAKUA KAMA YA MANGWEA
TUNASUBIRI KUSIKIA KUTOKA KWA NDUGU WA MAREHEMU KUHUSIANA NA SWALA ZIMA LA MAZISHI NA NAMNA MWILI UTAKAVYOSAFIRISHWA NA WAPI MAZISHI YATAFANYIKA.
MANGWEA KUSHOTO NA MARAFIKI NCHINI AFRIKA KUSINI SIKU CHACHE KABLA YA KIFO CHAKE
WAKATI HUO HUO MWANAMUZIKI MWANA FA ALIYEKUA ANATARAJIA KUFANYA SHOW SIKU YA TAREHE 31 ILIYOKUWA IMEBATIZWA JINA LA THE “FINEST” AMEFANYA MAAMUZI MAGUMU YA KUGHAIRISHA SHOW YAKE HIYO KWASABABU YA MSIBA HUO.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU aLBERT MANGWEA MAHALI PEMA PEPONI AMEN