Michelle Obama amekuwa kivutio cha wengi hasa linapokuja swala zima la jinsi anavyovaa, Kitu cha pekee na cha kuvutia kuhusu hili ni kwamba photoshoot ya issue hii imefanyika Whitehouse ambapo Michelle ameweka meengi wazi kuhusiana na mtazamo wake juu ya mitindo Hiki ndicho alichokisema Michelle kuhusu mitindo kwa wale wanaopenda mikato yake; “I always say that women should wear whatever makes them feel good about themselves. That’s what I always try to do. . . . I also believe that if you’re comfortable in your clothes it’s easy to connect with people and make them feel comfortable as well. In every interaction that I have with people, I always want to show them my most authentic self.” “Huwa nasema kuwa wanawake wanatakiwa kuvaa chochote ambacho kinawafanya wajisikie poa. Hicho ndicho kitu ambacho sikuzote mimi huwa nafanya….Pia naamini kuwa ukiwa unajisikia vizuri kwa kile ulichovaa ni rahisi kuungana na wengine na kuwafanya wajisikie vizuri pia, Katika kila nafasi nayopata kuunganika na watu, Siku zote napenda kuwaonyesha huu msingi wangu”.