Hatimaye Kanye West atangaza ndoa kwa Kim Kardashian, siku chache baada ya kujifungua mtoto wao wa kike ‘North West’
Ikiwa ni siku chache toka couple ya Kanye West na Kim Kardashian kupata mtoto wao wa kwanza wa kike ‘North West’ (June 15), hatimaye couple hiyo imeonesha nia ya kwenda ‘next level’ baada ya rapper Kanye kupropose ndoa kwa Star wa reality show ya “Keeping Up With the Kardashians” Kim Kardashian.
Kwa mujibu wa The Sun, wawili hao wanategemea kufunga ndoa yao mwezi September mwaka huu jijini Paris, Ufaransa.
Pamoja na kwamba Yeezy ametangaza ndoa kwa Kim bila kumvisha pete ya uchumba (engagement ring) kama ilivyoripotiwa, lakini inasemekana rapper huyo mwenye miaka 36 alitumia zaidi ya $500,000 kumnunulia mama North ‘black diamond ring’ kama zawadi ya kusheherekea kuzaliwa kwa mwanao wa kike North West.
Hatua hii ya Kanye kumwomba ndoa mama wa mtoto wake imekuja siku chache baada ya ndoa ya Kim na aliyekuwa mume wake wa pili Kris Humphries, kufikia tamati rasmi kisheria wiki iliyopita baada ya mvutano wa muda mrefu na Kris waliyekaa kwenye ndoa kwa siku 72 tu kabla Kim hajaomba talaka October (2011).
producer Damon Thomas ndiye alikua mume wa kwanza wa Kim toka mwaka (2000) mpaka (2004) ndoa ilipovunjika na baadaye kuolewa na Kris. Kanye West atakuwa mume wa 3 katika orodha ya wanaume waliowahi kufunga pingu za maisha na Kim, (hivi nimesema pingu za maisha? Kwa case ya Kris na Damoin nadhani niite pingu za muda!!).
Hope mara hii haitakuwa longolongo