Katika kuonesha kwamba bado ana kiu ya kuona sanaa yake inapanuka na kuvuma mbali huku akiboresha maisha yake, kukuza kipato na kuongeza ufanisi , msanii wa muziki wa kizazi kipya nchiniH. Baba ameamua kujikita katika biashara kwa style ya kipekee kwa kuingiza sokoni bidhaa aina ya pipi zenye jina, picha na chata zake, pipi zinazojulikana kwa jina la “H. BABA & FLORA MAPENZI KWA WATOTO”.
Pipi hizo zilizopambwa kwa picha ya H. Baba katika karatasi ya kuishika pipi, zikipambwa na mfuko wa nylon wenye uzito wa gram 250 uliona picha ya mwanamuziki H. Baba na mwigizaji wa Bongo movie Flora Mvungi na zinazo tengenezwa na kampuni yaTANFRIK LIMITED ya Nairobi nchini Kenya, tayari zimeanza kuuzwa kwenye baadhi ya maduka na vibanda mbalimbali vya biashara kanda ya ziwa.
pongezi nyingi kwa bonge la wazo kaka Hbaba Na Wifi