Wakiwa ni fresh wakitokea kushinda tuzo ya wimbo bora wa Reggae na Ragga katika tuzo za AFRIMMA, kundi hilo ambalo linabadilika badilika wawili hao walidhani mambo yalikuwa nirahisi kama kushinda tuzo waliyoipata. Team Radio na Weasel wataficha hii stori kwenye mioyo yao lakini mtandao wa How We unanusa kila mahali, wasanii hao kutoka Uganda walikutana na mshangao ambao hawakutegemea baada ya show yao kuudhuriwa na watu 30 tu huko Manchester nchini Uingereza. Wakali hao walipangiwa kufanya show mbili moja ilikuwa Manchester na nyingine Londoni, wasanii hao walipigwa na mshangao ambao wajawahi kukutana nao katika maisha yao, waliimba mbele ya watu 30. Ingawa hilo lilitokea lakini Radio na Weasel hawakushindwa kutoa burudani kwa mashabiki hao wachache waliohudhuria, show hiyo iliandaliwa na Ron Biggz na Mrz Biggz wa Miss Uganda UK. Lakini hii ni moja ya changamoto tu hakuna kilicho haribika, Radio na Weasel
ni kati ya wasanii wakali wanaokubalika sana Arfika Mashariki ndo maana waliweza kushinda tuzo za AFRIMMA tuzo ambazo zilifanyika siku si nyingi.