
ALBERT MANGWEA KULIA AKIWA NA MUSA AKA MOSSRED NA M TO THE P AMBAYE NAE INASEMEKANA AMRFARIKI DUNIA
Dr Shirley Radcliffe wa hospitali ya Helen Joseph ya jijini Johannesburg, Afrika Kusini, amethibitisha kwenye ripoti yake kuwa Albert Mangwea amefariki kutokana na “alcohol toxicity” (Alcohol intoxication ni hali inayotokana na matumizi makubwa ya pombe). Hiyo ni baada ya Mangwea kunywa sana pombe, kuchoka kupita kiasi na kutumia madawa ya kulevya kupita kiasi.
Inasemekana kuwa Albert, 28, alianguka nyumbani kwa marafiki zake na alikuwa amekunywa pombe zaidi ya mara tano ya kinachotakuwa kunywewa nchini Afrika Kusini ambapo kwenye damu yake kulipatikana 416mg za pombe kwenye kila milliliters 100.
Radcliffe ameeleza kuwa sababu ya Ngwair kupelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ni pamoja na hypoxia (upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye seli na tissue za mwili) na mmoja wa marafiki zake alipatikana na chumba mbili tupu za Vodka ziizokuwa kwenye gari.
Ripoti hiyo inadai kuwa Ngwair alikuwa na tatizo la kutokula chakula miezi kadhaa kabla ya kifo chake na pia kujirusha bila kupumzika hata kidogo. Sampuli zilizopatokana tumboni mwake zimeonesha mkusanyiko wa madawa ya kulevya mbalimbali yakiwemo Heroin,Cocaine ‘crack’ na bangi ya 0.08gms ilipatikana kwenye damu yake.
Kifo chake kilitokana na na mshtuko mkali wa moyo na kushindwa kupumua kulikotokana na moyo kuacha kufanya kazi na hivyo kupelekea kifo chake ndani ya sekunde chache tu.
——

6 Comments
Nickson msilu kutoka IRINGA.
Jamani dawa za kulevya sio ujanja jamani,
Tunawapenda sana na mnatuburudisha sana sasa haya mambo sisi mnatuachia majonzi hivi, badilikeni jamani.
Hata pombe sio ujanja ni ushamba tu, kunyweni kwa kipimo na kwa afya.
ripoti ya daktari haujatoka fake information shame
dada salama nakukubali sana, ngoja na mimi nitie neno hapa kwa upande wangu ngweir alikuwa mwanangu sana kwahyo lazima niguswe me bhana naona zake zilifika 2, wote tumuombee alazwe pema peponi amen
Mhmm! Watoto wetu jamani, wanaponzwa na kupendana umaarufu wa muda mufti. R I P Ngweair
Nothing much we can say, coz every one who lives, he will die, R.I.P our Bra..