Ma Ailun … aAlipokuwa hai na sare za kazi
Inarepotiwa kwamba kampuni ya APPLE watengenezaji wa simu aina ya iPhone 5 wameanza uchunguzi baada ya maisha ya mwanadada mrembo pichani kukatishwa na kichao daiwa shoti ya umeme iliyo tokana na simu yake aina ya iPhone 5.
Ma Ailun, 23, alipatwa na shoti ya umeme wakati akijibu simu yake ikiwa kwenye charge inarepotiwa. Ajali hiyo mbaya hadi kufikia kupoteza maisha ya mrembo huyo ilitokea Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Xinjiang Province nchini China.
Mrembo huyu ambaye alikuwa muhudumu wa kwenye shirika la ndege la China Sourthern Airlines na kuacha kazi hiyo hivi karibuni alinunua simu hiyo mwezi Desemba kweney duka la Apple nchini humo na alikuwa anatumia charger halisi ya Apple pia familia yake inareport.
Kaka yake amesema simu hiyo pamoja na charger yake vimekabidhiwa polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Mzungumzaji wa kampuni ya Apple amesema: “Tunasikitishwa sana na tukio lilitokea na tuanatoa pole kwa familia ya Ma Ailun. Tutachunguza kwa kina na kushirikaina kikamilifu katika uchungunguzi wa jambo hili.”
Tukio hilo limewapa wasiwasi watumiaji wa simu hiyo huku wataalam huko Hong Kong wakionya watu kuto tumia vifaa vyovyote vya umeme vikiwa kwenye charge (umeme).
Johnny Sin Kin-on, profesa katika chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia kilichopo Hong Kong amesema: “Kuna hatari ya kutumia kifaa cha umeme chenye betri wakati kikiwa kwenye charge (umeme), iwe shaver (kinyoleo) au simu.”
Simu aina ya iPhone 5 imekuwa imekuwa ikipokea malamiko mengi toka iingie sokoni kutoka kwa wateja wake. Malalamiko yalikuwa pamoja na ubunifu (utengenezaji) wake kutokuwa mzuri, charger yake pamoja na apps yake ya rami kutokuwa na ufasaha.
Wiki iliyopita iPhone 5 ilionekana kuwa ni simu ambayo imepoteza umaarufu na mauzo yake kushuka sana nchini Uingereza. Na katika test za Benchmark pia imeonekana kuwa na NUSU ya speed, ukilinganisha na simu aina ya Samsung Galaxy S4 ambayo kwa sasa iko juu sana.