
Jennifer Lopez ameweka wazi siri za mwili wake kuonekana ni kijana wakati wote, Jennifer Lopez (46) ambae anaonekana kama mwenye miaka 20 aliiambia US Weekly.
“Sinywi pombe, sivuti sigara au kunywa kahawa, hiyo kweli inaharibu ngozi yako unapokuwa mzee, tunakula mbogamboga, napenda kupika, napika vitu vingi, napenda kupika vyakula vya Kipuerto Rican kwa sababu ndicho kilicho nilea, J.Lo ambae amepaapa kutofanya upasuaji wa makalio yake au kwa ajili ya urembo mwingine alisema pia anao trainers wawili.
