Inaitwa Mv.Gold Star ilisajiliwa hapa Tanzania juzi Ijumaa imekamatwa nchini Italia ikiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya pauni milioni 50 sawa na shilingi bilioni 126. 5.
Watuhumiwa waliokuwa ndani ya meli hiyo waliamua kuichoma moto ili kupoteza ushahidi na kuamua kupiga mbizi majini lakini walitiwa nguvuni na wanausalama wa Italia.
ilikamatwa jirani na Kisiwa cha Sicilia katika Bahari ya Mediterranian nchini Italia wakati ikielekea Uturuki.