Kilichompata Madam Rita kinasikitisha! Ndivyo unavyoweza kusema ukibahatika kumuona the big boss wa Benchmark Production inayoratibu Shindano la Bongo Star Search, Rita Poulsen ‘Madam’ anayetembelea magongo baada ya kupata ajali mbaya ya gari.
Akizungumza baada ya kuwa kimya muda mrefu ikielezwa kuwa alipata ajali hiyo kitambo, Madam Rita alisema kuwa kwanza kabisa anamshukuru Mungu kwani anaamini kila kitu kinachotokea chini ya jua kina sababu yake na hata alipopata ajali hiyo alimshukuru kwa kutoka salama.
Madam Rita aliendelea kueleza kuwa ajali hiyo aliipata katikati ya Jiji la Dar na kusababisha kuvunjika kwa kifundo ‘enka’ cha mguu wa kulia hivyo kumsababishia kutembelea magongo baada ya hospitali kumuwekea ‘hogo’.
“Namshukuru Mungu kwanza kwa kunitoa salama katika ile ajali japokuwa sijapona vizuri,” alisema Madam Rita.
Mkurugenzi huyo aliendelea kueleza kuwa alipopata ajali hiyo alikimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili kwenye Taasisi ya Mifupa ya Moi lakini hali ilipokuwa kuwa mbaya alihamia katika hospitali moja ya Kichina ambapo kwa sasa amepata nafuu.