Huko morogoro Hali Ni Tete baada ya wananchi hawa wazawa Watanzania kuwekwa katika wakati mgumu kama wakimbizi, ni baada ya muwekezaji kuwavunjia Nyumba Zao
Wananchi hao wameilalamikia serikali kwa kushindwa kuwasaidia huku mwekezaji akiendelea kutumia nguvu kuvunja nyumba zao bila utaratibu..
mwekezaji huyo amechukua hekari zaidi ya 3000 kwa lengo la kufuga na kujenga majosho huku akivunja nyumba za wananchi walioishi kwa zaidi ya miaka 50 ambapo wamelalamikia kuathirika na kupata hasara na wengine kuibiwa mali zao zikiwemo fedha.