Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemtangaza Bwana RIDHIWANI KIKWETE mshindi wa kiti cha ubunge cha jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Akitangaza matokeo hayo baada ya wagombea wengine kupitia vyama vya CHADEMA, CUF, NRA na AFP kuridhia Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la C halinze Bwana SAMUEL SALIANGA aliesema Bwana RIDHIWANI KIKWETE amepata kura 20, 828 sawa na asilimia 86. 61, kati ya kura 24,422 zilizopigwa
Idadi hiyo ya waliopiga kura ni kati ya watu elfu 92 waliojiandikisha kupiga kura.
Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi Bwana RIDHIWAN KIKWETE amewashukuru wakazi wa Chalinze kwa imani walioionesha kwake na Chama Cha Mapinduzi na kuahidi kushirikiana nao kushughulikia matatizo ya ya jimbo hilo .
Hongera Sana