
Iggy Azalea anaonekana kwenye video akibishana na paparazzo nje ya supermarket huko Los Angeles.
Akiongeza list ya mastaa wengine katika uzoefu wa kukutana na paparazzi ambae alipenda kumfuatilia, Iggy Azalea alichuliwa video wikiendi iliyoisha akigombana na mpiga picha alikuwa akijaribu kumpiga picha kwenye supermarket huko L.A.
Video inaanza ikimuonyesha paparazzi na rafiki yake Iggy wakipigishana kelele kabla ya repa huyo ajaonekana akitoa maneno makali.
Mpiga huyo muda mfupi akasema ameshambuliwa na kuulizwa “Unaumwa ukimwi? Nina UKIMWi sasa labda na Ebola.
Repa huyo kutoka Australia anaonekana mwenyewe anaingia na kujibu, Sawa, Natumaini una Ebola, Natumaini unakufa. You are a f…..cunt!! Azalea anajaribu kumgonga mpiga picha huyo na vile trolley vya kubebea vitu supermarket (Pushcart) kabla hajapayuka, Unaingilia maisha yangu, Uko hapa wakati najaribu kununua mayai na unapiga picha, hivyo sivyo inavyotakiwa kuwa sweetheart, Hivyo ndivyo wanavyotaka? Unatia huruma…Hayo ni maongezi ya Iggy akizozana na Paparazi.
Repa huyo wa ngoma ya “Black Widow” anaendelea kugomba kwamba paparazzi huyo asingeruhusiwa kuwepo kwenye store hiyo
“Kuwa mwanamuziki haikupi haki ya kuingia supermarket na kumpiga mtu picha akinunua mayai, hiyo sio sehemu ya public, hii ni private, uko ndani ya store unapiga picha za watu sweetheart, sio sawa, haipendezi” alisema Iggy Azalea.
Wanaonekana wakitupiana maneno kila mmoja huku Iggy Azalea akionekana akiondoka na mpiga anamfuata anamwambia wewe ni mtu maarufu, mtu maarufu.
