Ukiwa ni mtu unaependa muziki ukisikia Camp Mulla lazima sio kitu kigeni katika masikio yako, Camp Mulla ni kati ya makundi bora yaliyotokea ndani ya miaka 10 iliyopita, walikuja, wakaona na kufanya vizuri bila shaka kabla ya kupotea katika ulimwengu wa burudani waliokuwa wameshaweka alama yao katika akili za watu na mashabiki baada ya kufanya mapinduzi katika muziki waliokuwa wakiufanya kwa sababu walikuja na muziki wa tofauti kabisa, baada ya stories kwamba kundi hilo lilitengana Lakini good newz ni kwamba kundi hilo linatazamiwa kurudi tena?
Mwaka wa 2015 unaokuja unaweza ukawa mwaka mkubwa kwao na studio watakayotumia ni ya Bruce Odhiambo katika eneo la Riara University. Hii no moja ya studio kali ambayo imebadilisha muziki kabisa ambao unasiklizwa nchini Kenya.
Inatengeneza ngoma kwa kila mtu ambae anatamani kuwaa maarufu. Inatoa mazingira mazuri kwa vyomboa vya habari kwa kutengeneza ngoma zenye ubora unaokubalika. Studio hiyo ina vyumba vitano bora vilivyotenezwa kwa kudhi mazingira ya studio, chumba cha mahojiano, control room, chumba cha kuingizi sauti (Vocal booth), chumba cha kueditia, chumba cha video na picha za kawaida.
Kwa hiyo tusubiri tuwaone kwa mara nyingine Camp Mulla kwenye kiwanda cha muziki baada ya kuwa pembeni ya gemu kwa muda usiopungua miaka mitatu, na Camp Mulla ni kundi ambalo lilisumbua sana na ngoma yao ya Fresh all day, wakaja Sauti Soul wamewarithi, Je Camp Mulla wataweza kuchukua nafasi yao? Tusubiri mwaka 2015 tuone itakuwaje….