Mwanaume huko nchini india inaelezwa amechangia mke na ndugu zake wa nne mbao wadogo zake na tayari wana mtoto mmoja, ambapo hata hivyo mtoto huyo hajulikani baba yake halisi ni nani.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la huko Uingereza, linaeleza kuwa mwanaume huyo ambaye alifahamika kwa jina moja la Gunddu alimuoa Rajo Verma mwenye umri wa miaka {21} miaka minne iliyopita, na Baada ya ya hapo ndipo akawa anawakaribisha ndungu kwaajili ya kuchangia mapenzi kwenye ndoa hiyo.
Akielezea maisha ya ndoa yake Rajo alisema kuwa yeye pamoja na wanaume zake huwa wanaishi kwenye chumba kimoja tu, Ambacho huwa wanalala kwenye mablanket ambayo huwa wanatandika chini, tofauti nawengi hufikiri huenda angekuwa anakitanda, jambo ambalo husema anapata starehe zaidi anapotandika Blanketi chini kwani anakuwa anapata raha awapo nawapenzi zake hao.
Rajo ana mtoto mmoja na wanaume hao, na kila siku hudai kufanya mapenzi na mwanaume mmoja tu kati ya wanaume 5, na jambo linalomshinda kuwa tofautisha na kufahamu mtoto ni wanani nikwamba wanaume hao wanafanana Mnoo, Alisema kwamba kilicho sababisha kuolewa na Shemeji zake hao nikutokana na Milla na desturi katika Kijiji kidogo kilichopo na jirani na mji wa Denhardin Kaskazini Mwa india, ambapo huwa mwanamke huolewa na shemeji zake.
Rajo alisema kuwa Mwanzoni Kilionekana kama kitu cha ajabu” Lakini Alikiri na kusema hana upendeleo kwa yeyote yule” Alisema Rajo.
Alidai kuwa mume wake wa kwanza kabisa katika kundi hilo la waume zake hao alikuwa Gunndu ambaye yeye walioana kwa mila za kihindu, Miaka minne iliyo pita, Ambapo rijo alisema kuwa Baadae aliolewa na na shemeji zake hao Ambao ni Baiju { 32 } Sant Ram{ 28 } Gopal { 26 } Na Dinesh { 19 }, Mume mwenye umri mdogo na aliye muoa Rajo ni { Denish } Ambaye pia alikuwa na miaka kumi na nane.
Kwamujibu wa habari zilizokuwa zimeelezwa na watu wa huko zinasema kuwa maeneo ambayo yanaendeleza mila na Desturi ya wanawake kuolewa na wanaume wengi ni yale ambayo yana idadi kubwa ya wanaume kuliko wanawake, Mila hizo zinaelekeza kuwa ndugu wa Mume wa kwanza wa Mke ndio wenye nafasi ya kumuoa mke wa kaka yao.
Rajo alisema kuwa alijua tu kwamba ataolewa na wanaume wengi, kutokana nakwamba mama yake nayeye aliolewa na shemeji zake wawili wa hiyo hakikuwa kitu kigeni kwake.
1 Comment
Aisee kama ingekuwa bongo huyu mama kuolewa wangesema nguvu zinatokana na kikombe cha Babuuuu…