
MWIMBAJI ambaye pia ni bosi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan Makongo ‘Mashauzi’, Jumatano iliyopita alikumbwa na masaibu mazito kufuatia kudakwa na polisi wa Kituo cha Msimbazi, Dar akituhumiwa kukwapua mkoba wenye kitita cha shilingi laki saba, elfu hamsini na nane na mia mbili (758,200) mali ya Veronica Tarik.
Chanzo cha habari kituoni hapo kilidai kuwa Jumanne iliyopita, Isha Mashauzi na shosti wake aliyejulikana kwa jina la Halima Shaban waliingia duka moja
Mtaa wa Mafia na Jangwani, Kariakoo, Dar kwa lengo la kufanya ‘shopping’ lakini walipochomoka, Veronica alishangaa kutouona mkoba wake.
Dida akiwa kituo cha polisi cha Msimbazi kwa ajili ya kumtolea dhamana
MashauziVeronica aliwakimbiza wawili hao na kuwadaka mtaa wa pili na kuwasomea tuhuma zao kisha akawaomba awasachi kwenye mafurushi waliyobeba lakini Isha na mshirika wake waligoma, hali iliyosababisha kuzuka kwa timbwili wakidai mwanamke huyo alitaka kuwadhalilisha.
Baada ya Veronica aliyekuwa na wapambe ‘legelege’ kuzidiwa nguvu, waligeuka na kukimbilia Kituo cha Polisi Msimbazi ambako alifungua kesi ya wizi kwa Isha na shosti wake kwa jalada namba MS/RB/4023/2013.
Maafande wenye difenda waliingia mitaani kuwasaka watuhumiwa hao mtaa hadi mtaa wakitumia mbinu mpya za kikachero na kufanikiwa kuwatia mbaroni Jumatano iliyopita.Isha akiwa selo, wapambe wake walimiminika kituoni hapo akiwemo Mtangazaji wa Kituo cha Redio Times FM cha jijini Dar, Hadija Shaibu ‘Dida’ kwa ajili ya kuhangaikia kuwachomoa wawili hao.

1 Comment
Watu hawaridhiki na asote rupango asipewe dhamana