Polisi wa nchini Sweden wamedai kupata dawa za kulevya katika basi linalotumiwa na mwanamuziki Justin Bieber anapofanya ziara zake za kimuziki.
Msemaji wa polisi Lars Bystrom amesema kiwango kidogo cha dawa za kulevya na silaha moja vimekutwa katika basi hilo wakati polisi walipolivamia likiwa halina mtu na kuegeshwa katika ukumbi wa Globen mjini Stockholm ambapo mwanamuziki huyo alikuwa akifanya shoo.
Polisi huyo amekata kutaja aina ya dawa zilizokamatwa akisema zimepelekwa maabara kwa uchunguzi.
Hata hivyo hakuna mtu aliyekamatwa.