Producer na Engeneer Chauncey Mahan amesema ni mmiliki wa albamu sita zilizotoka Roc-A-Fella Records., Jay Z na Roc-A-Fella wao ndo walengwa wakubwa katika kesi hii ya pili iliyofunguliwa na Chauncey Mahan imeripotiwa na TMZ.
Mahan amesema katika kesi hiyo mpya kwamba alikuwa producer tegemezi na kutengeneza album sita zilizoachiwa kutoka Roc-A-Fella wakati akiwa anafanya kazi na kampuni hiyo mwishoni mwa miaka ya 1990 na mapema 2000.
Na yeye ndiye aliyehusika sana kwenye sound katika album hizo zilizotoka na kufanya vizuri ikiwemo The life And Times of S.carter Vol 3…The Dynasty Roc La Familia ya mwaka 2000, ambazo zilitoka 1999 na 2000.
Chauncey Mahan anmtaka jaji kumfanya yeye kama mmiliki mwingine wa haki za kazi hizo ambazo zilitoakana na yeye kutengeneza.
Mwezi April Mahan alikamatwa baada ya kutuhumiwa kupanga kupiga mnada master tapes za Jay Z au azirudishe kwa Live Nation kwa dola 100,000 kama ada ya kuzihifadhi. Muwakilishi wa Jay Z alitoa malalamiko akilalamika mwzi Aprili kwa NYPD.
Lakini taarifa mpya zinasema kwamba Jay Z na Ro-A-Fella walipotezea malalamiko hayo kwenda kwa Chauncey.