Lil Wayne amethibitisha kwamba Drake atakuwepo kwenye baadhi ya nyimbo za albam ya Tha Carter V, Nick Minaj pia yuko kwenye list ya wasanii watakaosikika kwenye The Carter V. Lil Wayne ambae amepanga kuwepo na Drake kwenye Tour yake mwaka huu, amefunguka na kuweka wazi mashabiki wategemee nini.kutoka kwa wasanii hao wawili kutoka Young Money.
“Mpango unakwenda, Namshukuru Mungu, tumefanikiwa sana, nenda mbele rudi nyuma na ngoma zetu zilifanya vizuri, tunafanya umati upagawe, alafu mwisho wake tunatokea kwenye stage pamoja inakuwa ni nom asana nadhani ni kitu Fulani hivi kama tunashindana stejini” Alisema Lil Wayne wakati akipiga stories na MTV.
Lil Wayne aliulizwa anadhani nani atashinda alisema anamuwekea mipaka. Lil Wayne na Drake tayari wameshasikika kwenye ngoma ya Believe Me, Lil Wayne amesoma kuna ngoma kibao zinakuja kutoka kwa wawili hao.
Msanii mwingine aliyepangwa kuwepo katika albamu hiyo ni Nick Minaj, pia Lil Wayne atakuwepo kwenye The Pink Print ya Nick Minaj. Haziwezi kuwa albamu bila wao kuwepo..Alisema Boss huyo wa Young Money Lil Wayne..
Tour ikishatangazwa utapata infos zote kupitia salmamsangi,cim kama Lil Wayne Vs Drake Tour inacross nearby your city.