
Mwanamuziki mwenye umri wa miaka 21 kutoka Canada mwenye matukio kibao, kipenzi cha wakinadada Justin Bieber ameomba msamaha na kujutia baada ya kutumia lugha iliyoonyesha ubaguzi wa Rangi, Mwanamuziki huyo sio mgeni katika kuomba msamaha, alishaomba msamaha kwa kupiga teke bendera ya Agentina na alisema ilikuwa ni bahati mbaya.
Pia alishawahi kuomba msamaha kwa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton baada ya kuonekana kwenye video akispray picha ya rais huyo huku akisema maneno ambayo huwezi kuyasema , video hiyo ilipostiwa kwenye mtandao wa TMZ.
Na mapema mwezi huu wa Juni aliomba msamaha sio mara moja ila ni mara mbili baada ya kutoa maneno yanayoashiria ubaguzi . Matukio ya ubaguzi wa Rangi yamekuwa mengi sana pia mmiliki wa timu ya basketball Donald Sterling nae kitu kama hiki kilimtokea.
