
Kanye West amezomewa kwa mara ya pili ndani ya siku mbili wakati akiperform kwenye tamasha linaloitwa Wireless Festival, West alizomewa Ijumaa baada ya kuimba sehemu ya Drake ambaye alikuwa akiumwa na aliendelea zaidi ya dakika 20 akiwa kwenye jukwaa na aliwafanya mashabiki wapige kelele huku wakisema tunamtaka Drake lakini muda ulivyokuwa ukienda akiendelea kuimba watu wakarudi na kuanza kumshangilia.
“Mimi katika maisha ya ukweli na aibu sana, kwa sababu na aibu sana kufanya vitu vya kijinga, muda mwingine ni ngumu kwa sababu na aibu sana kuwa na mambo mengi, najivunia na na aibu na kidogo niko legelege, naona aibu sana kudanganya kwa mtu yeyote na najiamini zaidi mimi mwenyewe kufanya nidanganye kwa sababu uongo una kazi sana. Vyombo vya habari vinajaribu kunishusha kunifanya nionekane kama mimi ni kichaa lakini najituma sana kufanya huu muziki na nyie wote kuusikiliza na najua mwisho wa siku wote nyie ni wa kwangu na hilo ndo la muhimu. Sababu muhimu kwanini nipo kwenye steji hii ni kwa sababu wote nyie ni watu wangu, Mnajua naenda studio mpaka saa 9 usiku hiyo ni sababu unasikiliza muziki kwenye gari lako” Alisema Kanye.
