
Kelvin Adorno mwenye umri wa miaka 28 ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Bevy Promotions &Media ameuawa kinyama na mtu asiye na makazi wakati alipokuwa njiani akitokea Marryland kuelekea Miami, Florida kwa ajili ya kuomba uchumba kwa rafiki yake wa kike wa muda mrefu.
Akiwa njiani kuelekea nyumbani kwa mpenzi wake huyo huku akitumia usafiri wa baiskeli, Kelvin aliamua kuingia latika mgahawa wa McDonald. Akiwa nje ya mgahawa huo aliamua kumpigia simu mpenzi wake na wakati akiwa anazungumza kwenye simu alijitokeza mtu asiye na makazi na kumchoma visu hadi alipokumbwa na mauti.
Polisi walikuta pete ya uchumba katika mfuko wa shati wa Kelvin wakati mwili wake ulipopatikana nje ya mgahawa huo wa McDonald. Polisi walifanikiwa kumkamata muuaji huyo mwenye umri wa miaka 59 ambaye aliwaambia polisi kuwa alihisi kuwa Kelvin alikuwa akipanga kumuua.
Kelvin akiwa na mpenzi wake enzi za uhai wake
