
Kwa sasa unaweza kusikiliza albamu ya mwanadada Keyshia Cole inayoitwa “Point of no return” kupitia U Stream. Mwanadada huyo ameonyesha cover art ya albamu hiyo kupitia Rap-Up.
Cover hilo linamuonesha Keyshia Cole akiwa amevaa miwani na jeans amekaa juu ya gari alafu ikionekana barabara ambayo hakuna kitu chochote.
Ngoma ambayo ameiachia kuitangaza albamu hiyo inaitwa“Rick James”akiwa amemshirikisha Juicy J na production ni ya DJ Mustard.
Wale, Future na 2 Chainz ni kati ya wasanii ambao wameshirikishwa kwenye albamu hiyo pamoja na Mario Winans na Mike WiLL Made-it
Kwa sasa Keyshia Cole ameongea na Fuse kuhusu Point of No Return.
“Kabisa kuna ngoma kali kwenye hii albamu ambazo sijawahi kufanya, Nafurahishwa kuona watu wanafikiria kuhusu hilo, tutaona jinsi gani watu wataipata albamu, nadhani ni albamu kali na nahisi ni moja ya albamu zangu kali kwa leo” alisema Keyshia Cole.
Albamu ya “Point of no return” ilitangazwa kutoka siku ya jana Oktoba 7, August Alsina ni msanii mwingine ambaye anapatikana kwenye albamu hiyo production nyingine ni Stargate taarifa kwenda kwa waandishi wa habri zimeeleza. Na nyimbo zinazopatikana katika albamu ya “Point of no return” ni
1. “Intro (Last Tango)”
2. “Heat of Passion”
3. “N. L. U” (feat. 2 Chainz)
4. “Next Time” (Won’t Give My Heart Away)
5. “Rick James” (feat. Juicy J)
6. “Do That For (B.A.B.)”
7. “New Nu”
8. “She”
9. “Believer”
10. “On Demand” (feat. Wale & August Alsina)
11. “Love Letter” (feat. Future)
12 “Party Ain’t a Party” (feat. Gavyn Rhone)
13. “Remember (Part 2)”
