Msanii Mkongwe wa kizazi kipya Lady Jay Dee Jana Alipamba vichwa vya habari vya mitandao mbali mbali ya kijamii baada ya Viatu Vya thamani alivovinunua kwa thamani ya shilingi laki moja stini na nane kutaka kumdondosha wakati aki toa burudani katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika jijini Dar es salaam
Sababu ya wengi ku notice gharama za viatu hivyo na kugundua kuwa ni vipya ni baada ya Lady Jay dee kuvionyesha wakati anavinunua katika kipindi chake cha Diary ya Lady Jay Dee
Hata hivyo Jide alitumia mitandao ya jamii kuelezea swala hilo
Kupitia facebook aliandika” KUANGUKA JUKWAANI NI AJALI KAMA AJALI NYINGINE,ISITOSHE SIKUANGUKA BALI NILIKARIBIA,ILA POLENI KWA MLIOUMIZWA NA HICHO KITENDO…NITAPUNGUZA UREFU WA VUATU SIKU NYINGINE.
Pia Alitweet ” NI BAHATI MBAYA TU, KWANI HATA MWANZA, KAHAMA, DODOMA VILIKUWA VIREFU KAMA HIVYO HIVYO NA SIKUTEGUKA”
1 Comment
It happens dear we understand, love u.