
Kuna mkutano ambao ulifanyika Jumanne baada ya mchekeshaji Robin William kujiua, na watayarishaji wa filamu yake ya mwisho wanajaribu kuamua kama watafuta sehemu ambayo inamuhusisha Robin akiwa amecheza kama mlevi.
Filamu hiyo ni ya family friend comedy lakini wakati wa kipande kimoja anaonekana Robin na mtoto wake , imechezwa na Joel McHale inamuonesha Robin kama mlevi ambae ameacha pombe kwa miaka 6, wakati katika maisha ya ukweli Robin alikwenda rehab kwa miaka sita kabla ya umauti kumkuta.
Katika mkutano huo uliofanyika jana watayarishaji hao wa filamu hiyo wameamua filamu hiyo ibaki kama ilivyo.
Chanzo cha taarifa hii kwa Watayarishaji wanasema wkati wiki 4 Robin alikuwa kwenye set mwezi April 2013, alikuwa soba kabisa na hakuonyesha dalili za msongo wa mawazo, kitu ambacho kumbe haikwa hivyo, alikuwa na furaha kipindi chote cha kufanya filamu hiyo.
Taarifa zinasema kutakuwa na badiliko moja kwamba picha ya Robin itaonekana mwsiho kabisa kama kumbumbukumbu yake.
