
Hii Dunia Imefika mwisho Kabisa yani Mwisho sana… Bara La Asia Limekua Ni bara linalokubwa na maafa makubwa sana kila kukicha, kama matetemeko ya ardhi, Mafuriko, Vimbunga Nk… Wana Geographia wanatupa sababu za Namna Miamba bahari na uumbaji wa dunia ulivyo lakini tukiwaza sana tunaweza sema huenda haya wayafanyayo ndio chanzo cha yote kwa kumuudhi mungu kwa kiasi kikubwa
Sitaki sema mabara mengine yapo perfect lakini Bara Hili Lina Zaidi ya mambo yasio yakawaida
Hivi Karibuni Huko Korea Ya Kusini kulitolewa sheria ya kuwashurutisha na kuwalazimisha watu kwenda safari za mapumziko ili kuzalisha watoto tena ikiwezekana hata kukodisha wanaume, na hivi karibuni tena wakapitisha sheria ya kupangisha wanaume yani unamchukua mwanaume kwa muda kwasababu ya haja yako kisha mkimalizana ndo yameisha
Sasa hivi wamekuja na lipya Kabsaa baada ya kuhalalisha kisheria UZINIFU ..lakini wenyewe wanasema sio kwa ubaya.
Katika kikao cha mahakama ya kikatiba ya korea ya kusini ambacho kilifanyika jana tarehe 25.02.2015 waliitengua sheria iliyodumu kwa takribani miaka 60 iliyokuwa ikikataza matendo yote ya uzinifu na kuadhibu watu wenye hatia kwa miaka miwili ya jela.
