Wanawake wa kichina wanaokwenda nchini Korea Kusini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kubadili muonekano wao kwa madaktari bingwa wa plastic surgery wamejikuta katika wakati mgumu katika sehemu za usalama za viwanja vya ndege wakati wa kurudi China kutokana na operations hizo kubadili kabisa uhalisia wa sura zao ikilinganishwa na picha zao zilizopo kwenye passport kabla ya kufanyiwa operations hizo. Operation hizo zimesababisha wanawake hao kushindwa kutambulika kabisa na maafisa wa usalama,Katika kukabiliana na tatizo hili madaktari wanaowafanyia plastic surgery wanawake hao wanafikiria kuwapa vyeti vya kuwatambulisha wanawake hao vitakavyokuwa
na namba za passport zao, majina ya hospitali walizofanyiwa upasuaji huo pamoja na muda waliokaa Korea, ili kuwasaidia wanawake hao waweze kurudi tena nchini kwao China.