Mwaka 2006 repa Yung Joc ambae alikuwa na ngoma iliyofanya fresh ya “Tt,s going down” ilikuwa namba 20 katika list ya Forbes.
Katika mahojiano aliyofanya jana amesema hicho kilikuwa kitu cha hatari sana kwake, lakini sababu yake aliyotoa inafurahisha kidogo.
“Ile ilikuwa kitu kikubwa na kibaya ambacho kimewahi kunitokea kimenitokea, Unakuta wanakuja watu wanataka kukukopa dola 1,000 mara huyu hiki, ambapo nilikuwa naweza kuwapa, na baada ya kutokea vile niko katika List ya Forbes walikuja washkaji wanataka mkwanja mrefu zaidi, anakuja mtu anasema unaweza ukanikopa dola 10,000, Nikawa nashangaa kumbe watu walijua nimevuta mkwanja mwingi sana, Ikitokea mimi kwenda kutaka kitu watu wanashangaa!! vipi wewe umepata dola milioni 10 unaomba nini tena? ilisababisha watu wanishangae, kitu hicho kilifanya watu wawe na hasira na mimi waliona kama nafanya makusudi, sikuwahi kuona kitu kama kile katika maisha yangu” Alisema Yung Joc.