Leo nauthibitisha ule usemi wa Nabii hathaminiwi kwao na kweli naamini sasa kila mtanzania ni Star… Pamoja na Feza kutuwakilisha vizuri sana katika shindano la Big Bother The Chace kule Afrika kusini lakini alipata mapokezi hafifu sana toka kwa watanzania kwani walioonekana uwanjani walikuwa ni ndugu zake tu na rafiki
Mambo ni tofauti mara baada ya Feza kuwasili Nchini Botswana anapotokea mpenzi wake Oneil waliyekutana nae ndani ya Nyumba Hiyo…Feza alipokelewa kama ndiye mshindi kutika shindano hilo wakati ni mgeni tu wa mshiriki mwenzie ambaye mioyo yao iligongana ndani ya nyumba ya the Chase
Hivyo ndivyo picha za mapokezi ya Feza Ukweni zinavyojionyesha toka uwanja wa ndege mpaka mtaani.