Leo Juni 16 2014 kila mwaka huadhimishwa siku ya mtoto wa Afrika, Baadhi ya watoto nchini Tanzania wameitumia siku ya mtoto wa Afrika kuiambia jamii kwamba ihakikishe inawapa nafasi ya kusikilizwa ma kushirikishwa katika mambo mbalimbali.
Katika haki ambazo mtoto amekuwa akidhulumiwa na haki ya kusoma, kucheza, kusikilizwa na kuishi, ukatili dhidi ya watoto umekuwa ukiendelea sehemu mbalimbali katika nchi yetu hivi juzi tumetoka kusikia sakata la mtoto Nasra ambae aliishi ndani ya box kwa miaka minne na hatimaye kukatisha maisha yake, hapo amekoseshwa haki yake ya kuishi.
Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009, inataja haki za mtoto kuwa ni pamoja na kulindwa dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote,kupata chakula bora, malezi bora, huduma za afya, elimu, uhuru wa kuamua na kushirikishwa kufanya maamuzi, kucheza na kupumzika.
Sheria ya mwaka 2009 ya mtoto inaeleza haki za mtoto kwamba ni pamoja kupata elimu, chakula bora, kuliindwa dhdi ya ubaguzi, huduma za afya, uhurua wa kuamua na kushirkishwa katika kuamua mambo pamoja na kupumzika.