Lile jinamizi la kuteteteza mahusiano ama ndoa za mastar wa hollyWood limeendelea kwa kasi ya ajabu na sasa hivi linanyemelea ndoa ya mcheza sinema Halle Berry na hii itakuwa ni ndoa yake ya tatu kuvunjika
Baada ya ndo ayake ya awali kuvunjika halle alisema anaogopa sana kufunga tena ndoa lakini baada ya kukutana na Eric Benet alibadili mawazo yake na kuamua kuondoa hofu hatimae akafunga tena ndoa, Lakini kama hofu yake ilivyomuambia pale awali kweli ndo ahiyo haikudumu na badala yake ikavunjika tena Halle akaapia kutofunga ndoa tena lakini kwa mara nyingine tena akavunja miiko yake na kuamua kufunga ndoa alipokutana na Olivier Martinez
Inaonekana uoga wake unamaana sana japo anauzembea kwasababu hatimae ndoa hii nayo inachechemea
Ripoti toka jarida la Star ni kwamba Halle Berry na mme wake wa sasa Olivier Martinez mambo yameanza kwenda mrama , jarida hilo limesema wanandoa hao wote wakiwa na umri wa miaka 48 na wazazi wa Mtoto Marco mwenye umri wa miezi 10 wamekuwa wakiisha tofauti kwa miezi miwili sasa
“Hawazungumzi sana pamoja tena, na kama watafanya hivyo basi ni kwa ajili ya mtoto wao” ripoti hiyo ilisema