Maelfu ya waandamanaji wameingia barabarani mjini Paris hii katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa kuwa madarakanai Rais Francois Hollande (pichani) wakimshutumu kwa kuupa kisogo siasa za mrengo wa kushoto.
Katika mkesha wa kuadhimisha ushindi wa Hollande wa Mei 6 mwaka jana dhidi ya aliyekuwa rais wa siasa za mrengo wa kulia Nicolas Sarkozy, upande wa siasa za mrengo wa kushoto unaoungwa mkono na viongozi wa Kikomunisti wamewakusanya wafuasi wao kwa maandamano kunzia Bastille, ambao ni ukumbi maarufu katika vuguvugu la mapinduzi ya Ufaransa.
Watu wengi pia walitarajiwa kufanya maandamano tofauti mjini Paris na miji mingine ya kuipinga mipango ya serikali ya kuidhinisha ndoa za jinsia moja na kuwaruhusu mashoga kuwalea watoto.
Maandamano hayo yanakuja wakati uchunguzi wa maoni ukionesha kuwa Hollande ndiye rais asiyependwa na raia wengi wa nchi hiyo katika historia ya karibuni-DW.